Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kupeleka mahema Benin kufuatia mafuriko

UM kupeleka mahema Benin kufuatia mafuriko

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR juma hili limeaanza kusafirisha kwa dharura mahema kwenda nchini Benin taifa lililo Afrika Magharibi wakati linapoendelea kushuhudia mafuriko mabaya zaidi ambayo hayajatokea kwa miongo kadha.

Mahema 3,000 yatasafirishwa kutoka nchini Denmark ili kutoa makao kwa takriban watu 680,000 walioathirika na mafuriko. Thuluthi mbili ya Benin imeshuhudia kiasi kikubwa cha mvua wakati karibu visa 800 vya ugonjwa wa Cholera vikiripotiwa. George Njogopa anaarifu zaidi

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Maturubai hayo ambayo kiasi cha 3,000 yanatazamiwa kusafirishwa kutoka nchini Denmark yanatazamia kuwafikia zaidi ya wait 680,000 ambao wamekosa makazi.

Afisa wa shirilka la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya binadamu OCHA amesema kuwa misaada zaidi inahitajika ili kuwafikia mamia ya raia wanaoendelea kuathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha. Vyombo vya hali ya hewa vimesema kuwa hakuna dalili inayoonyesha kwamba mvua hizo zitafikia ukomo lini.