Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 100 wahofiwa kuathirika na kipindupindu Haiti

Watu zaidi ya 100 wahofiwa kuathirika na kipindupindu Haiti

Watu 150 wameripotiwa kuaga dunia nchini Haiti kufuatia kutokea kwa mkurupuko wa ugonjwa unaokisiwa kuwa wa kipindupindu katika eneo la Artibonite.

Watu wengine 1500 wanaripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo . Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini ikiwa ugonjwa huo ni kipindupindu baada ya Haiti kutoshuhudiwa maradhi hayo kwa karibu karne moja.

Kwa sasa mashirika la  afya dunia WHO na la kuhudumia watoto UNICEF yametuma madawa kwenda kwa maeneo yaliyoathirika.