Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa vya polio vimeongezeka miongoni mwa watoto nchini Pakistan :

Visa vya polio vimeongezeka miongoni mwa watoto nchini Pakistan :

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema visa karibu 80 vya polio vimeripotiwa nchini Pakistan.

Visa hivyo vimebainika katika majimbo mawili ya Kaskazini mwa nchi ambayo yaliathirika vibaya na mafuriko ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF Marixie Mercado , shirika hilo limekuwa likiunga mkono na kusaidia kampeni za chango ili kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema kumekuwa na ongezeko la idadi ya visa vya polio vinavyoripotiwa miongoni mwa watoto, na kumekuwa na visa 78 tangu Oktoba 14, ambavyo ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2009. Visa hivi ni licha ya kwamba UNICEF imekuwa ikisaidia kampeni ya chanjo ambayo hadi sasa imewashawafikia watoto zaidi ya milioni 8.5.