Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu bilioni mbili kuwa na mtandao mwisho mwa 2010:ITU

Watu bilioni mbili kuwa na mtandao mwisho mwa 2010:ITU

Takwimu mpya za kitengo cha mawasiliano cha kimataifa ITU zilizochapishwa leo zimeonyesha kwamba idadi ya watu wanaotumia mtandao wa internet duniani kote imeongezeka mara mbili katika miaka mitano iliyopita.

Takwimu hizo zinasema inategemewa kuwa idadi hiyo itafikia bilioni mbili ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2010. Idadi ya walio na uwezo wa kutumia mtandao wa internet majumbani kwao imepanda kutoka bilioni 1.4 2006 hadi bilioni 1.6 mwaka huu.

Takwimu hizo zimetolewa leo ikiwa ni mkesha wa kuamkia siku ya takwimu duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Oktoba 20. Watu milioni 162 kati ya milioni 226 ambao ni watumiaji wapya wa internet mwaka 2010 watakuwa wanatoka nchi zinazoendelea ambako matumizi ya internet yanaongezeka kwa kiwango kikubwa. Susan Telcher ni mkuu wa kitengo cha takwimu cha ITU.

(SAUTI YA SUSAN TELCHER)

Ifikapo mwishoni mwa mwaka huu asilimia 71 ya watu wote katika nchi zilizoendelea watakuwa katika mtandao ukilinganisha na asilimia 21 katika nchi zinazoendelea. Asilimia 90 ya watu katika nchi 143 duniani wanamudu huduma ya simu za mkononi na wengi ni kwa kutumia mtandao wa 3G.