Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa barani Ulaya Ban amesisitiza haki kwa wote na kuonya juu ya siasa za kibaguzi

Akiwa barani Ulaya Ban amesisitiza haki kwa wote na kuonya juu ya siasa za kibaguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia bunge la muungano wa Ulaya hii leo amesema Umoja wa Mtaifa na muungano huo ni washirika katika kupambana na matatizo makubwa yanayoikabili dunia.

Ban ametoa wito wa kuchukua hatua za pamoja kupambana na umasikini, mabadiliko ya hali ya hewa na kutokomeza silaha za nyuklia. Wakati huohuo ameonya wanasheria mjini Strasbourg Ufaransa dhidi ya siasa mpya zinazohusiana na masuala ya uhamiaji huku wahamiaji wa kiislamu wakiwa walengwa.

Hii ni kusistiza ujumbe kuhusu kuvumiliana na kutobaguana alioutoa awali kwenye sherehe za miaka 60 za mkataba wa Ulaya wa haki za binadamu, alipohutubia baraza la muungano wa Ulaya.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Amesema haki za binadamu kwa wote sio ndoto, na ametoa wito wa kuunga mkono watetezi wa haki za binadamu, makundi ya jumuiya za kijamii na vyombo vya habari ambao mara kadhaa wako kwenye hatari, wao na familia na marafiki zao kwa ajili ya kutetea haki za binadamu.