Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufanisi wahitajika kwa makampuni ya ulinzi Afghanistan:UM

Ufanisi wahitajika kwa makampuni ya ulinzi Afghanistan:UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya ulinzi kwa makampuni binafsi amekaribisha report ya uchunguzi inayohusu kampuni mmoja ya kimarekani inayofanya kazi huko Afghanistan akisema kuwa angalua sasa wamepata pahala pa kuanzia.

Hivi karibuni, kamati iliyoundwa na maseneta wa Marekani ambayo ilikuwa na kaazi ya kuchunguza namna makampuni ya ulinzi yanayoendesha kazi zake huko Afghanistan, ilibaini baadhi ya maeneo yakiwa na mapungufu makubwa. George Njogopa na habari zaidi

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kamati hiyo katika report yake ilisema kuwa, makampuni ya ulinzi ya kimarekani yaliyopewa kandarasi huko Aghanistan yanakabiliwa mapungufu mengi ikiwemo kukosekana umakini wa kazi, na wakati mwingine makampuni hayo yanaajiri wafanyakazi bila hata kuwafanyia uchunguzi wa kina.

Akizungumzia kuhusu report hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wataalamu kwenye fani hiyo Alexander Nikitin ameseama ipo haja sasa kuanza kuyafanyia kazi yale mapungufu yanayojitokeza mara kwa mara. Ameshauri kwa mamlaka husika ambazo zinatoa kandarasi kwa makampuni binafsi kuweka mifumo na kanuni za udhibiti kwa ajili ya kuleta uwajibikaji kwenye maeneo ya kazi