Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la watu mashuhuri la UM latoa wito kujitolea kuleta maendeleo kwa nchi masikini

Kundi la watu mashuhuri la UM latoa wito kujitolea kuleta maendeleo kwa nchi masikini

Mwanachama mmoja wa kundi la watu mashuhuri walioteuliwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kungalia matatizo ya kimaendeleo yanayozikabili nchi maskini duniani amesema kuwa nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea ni lazima zijitolee katika kupunguza umaskini ili kufanikisha juhudi hizo.

Alpha Oumar Komare rais wa zamani wa Mali na mwemyekiti wa kundi hilo la watu mashuhuri la UM kuhusu nchi maskini amesema kuwa jamii ya kimataifa inastahili kujitolea kifedha kusadia nchini zinazoendelea na pia kuwepo kwa kwa ushirikiano katika kupambana na ufisadi kwenye nchi hizo.

Akiongea na waandishi wa habari baada mkutano wa kwanza kundi hilo bwana Konare amesema kuwa wafadhili pia wanahitajika kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa fedha wanazotoa zimetumika kwa njia inayofaa.

Ban amesema kuwa tajriba waliyopata wanachama hao inawaweka katika nafasi nzuri kabla ya mkutano wa UM kuhusu nchi maskini mjini Istanbul nchini uturuki mwezi mei mwakani. Ban amesema kuwa mkutano huo utajadili hatua mpya kwa nchi maskini katika masula ya misaada, bishara, uwekezaji, teknolojia pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.