Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la maendeleo afrika limeanza rasmi Addis Ababa

Kongamano la maendeleo afrika limeanza rasmi Addis Ababa

Kongamano la saba la maendeleo barani Afrika limefunguliwa rasmi hii leo kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Kongamano hilo litakalomalizika Oktoba 15 limeandaliwa na Bank ya maendeleo Afrika ADB, Umoja wa Mataifa, tume ya maendeleo kwa ajili ya afrika (UNECA) na Tume ya muungano wa Afrika (AUC), ili kushughulikia changamoto za maendeleo zinazolikabili bara hilo na kisha kupata muafaka kwa ajili ya ajenda ya maendeleo.

Miongoni mwa changamoto hizo ni mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la idadi ya watu, afya, usawa wa kijinsia, masuala ya wanawake na, vijana na watoto. Mme Akila Belembaogo ni mwakilishi wa UNICEF kwenye tume ya uchumi ya Muungano wa Afrika.

(SAUTI YA MME AKILA)

Miongoni mwa wanaohudhuria ni pamoja na mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wataalamu wa maendeleo, jumuiya za kijamii na makundi mbalimbali.