Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kupiga picha dunaini "One day on Earth" kuandaliwa

Mradi wa kupiga picha dunaini "One day on Earth" kuandaliwa

Watu kote duniani wanaoshirika kwenye mradi unaofahamika kama "One Day on Earth" wanatajiwa kunasa picha za video kwa wakati mmoja kwa muda wa masaa ishirini na manne.

 Washiriki wanao wajumuisha vijana na watengeza vipindi watatumia kamera za kisasa na kuupiga picha kote ulimwenguni. Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limeshirikiana na mradi huu ili kuuwezesha kuwafikia washiriki kwenye nchi mia moja na kuufanya kuwa wa dunia nzima.

Kwa sasa mradi wa "One Day on Earth" unaendela kuwashirika maelfu ya watengeza filamu na wananchi wengine kutoka nchi 190. Matokeo ya mradi huu ambao utakusanya matukio ya kila aina yakiwemo ya kushangaza na kuogofya yanayofanyika kila siku sehemu mbali mbali duniani yatatumika kuunda makala ambayo itatolewa mwaka ujao.

Wakati ulimwengu unaendelea kujitahidi kutekeleza malengo ya mileni mradi huu pia utasaidia kuonyesha vizuizi vinavyo kabili baadhi ya nchi zitakazoshiriki katika kuafikia malengo hayo.