Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

G77 wasisitiza jukumu la utawala wa kimataifa:Ban

G77 wasisitiza jukumu la utawala wa kimataifa:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema uongozi wa kundi la nchi zinazoendelea zijulikanazo kama G77 na Uchina wametoa msisitizo kuhusu jukumu la Umoja wa Mataifa katika utawala wa dunia.

Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa mawaziri wa kundi hilo mjini New York hii leo Ban amesema amefurahi na kuridhika kwamba mada hii ya utawala wa kimataifa imejadiliwa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu amesema mtihani mkubwa ni kwa kiwango gani Umoja wa Mataifa G77 na Uchina watapiga hatua kwa upande wao kwenye ajenda za amani, maendeleo na haki za binadamu.

Amesema hakuna kinachoweza kulinganishwa na uwep wa Umoja wa Mataifa. Tuna wanachama wengi na wanaweza kuhakikisha kwamba mataifa madogo na yasiyo na nguvu yanakuwa na sauti katika sheria na maamuzi ya kimataifa. Lakini lazima tuendelee kulinda amani. Hii inamaanisha uratibu na mawasiliano yawe mazuri zaidi.