Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa ICG kuhusu Somalia wamalizika Madrid

Mkutano wa ICG kuhusu Somalia wamalizika Madrid

Mkutano wa 18 wa kundi la kimataifa liitwalo International Contact Group, ICG kuhusu Somalia umemalizika leo mjini Madrid Hispania.

Mkutano huo uliohuduriwa pia na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed umefanyika chini ya uwenyekiti wa Dr Augustine Mahiga ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.

ICG imesema msimamo wake kuhusu Somalia uko palepale na mkutano huo umetoka na mikakati kadhaa ya kufuatilia ili kufanikisha nia ya kuleta amani ya kudumu nchini humo. Jason Nyakundi anayo taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)