Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa shirika la UNESCO alaani mauaji matangazi wa habari wa runinga nchini Iraq

Mkuu wa shirika la UNESCO alaani mauaji matangazi wa habari wa runinga nchini Iraq

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amelaani mauaji ya mtangazi mmoja maarufu wa runinga nchini Iraq.

Riad al - Saray mtangazaji wa masula ya kidini na kisiasa kwenye kituo cha runinga cha al-Iraqiya alipigwa risasi na kuwawa na watu wasiojulikana mjini Baghdad mapema juma hili. Bi Bokova amesema kuwa mashambulizi kama hayo dhidi ya waandishi wa habari ni kama mashambulizi dhidhi ya haki ya kuzungumza na kwa jamii kwa ujumla. Bokova ametoa wito kwa serikali ya Iraq kufanya kila juhudi kuwachukulia hatua wahusika ili kuboresha usalama kwa wafanyikazi wa vyombo vya habari.

Kulingana na ripoti kutoka kwa waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka ni kuwa waandishi wa habari 230 na wafanyikazi wengine katika sekta ya mawasilion wameuawa nchini Iraq tangu mwezi machi mwaka 2003.