UNICEF imezindua kampeni nyingine ya machanjo huko Haiti

31 Agosti 2010

UNICEF inakadiria kwamba zaidi ya watu milioni 2 wangali wanaathiriwa moja kwa moja au kwa njia nyingine na matokeo ya mtetemeko wa ardhi huko Haiti. Na watu wengine milioni 1.3 wamekoseshwa makazi yao hadi hivi sasa.

Kwa upande mwengine shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM na kampuni ya Digicel zimeanza kampeni muhimu ya kuwashauri wa Haiti kupitia ujumbe wa SMS juu ya namna ya kujitahadhari kutokana na msimu wa kimbunga.

Mwakilishi wa IOM huko Haiti Jean Philipe Chauzy anasema kwa vile msimu wa kimbunga umeanza, juhudi zao ni kuwasiliana na watu ambao tayari wameathirika na tetemeko la ardhi la Januari 12.

"Kama tunavyo fahamu chama cha Msalaba Mwekundi cha Haiti na idara ya wakazi wamebuni mfumo wa kutoa habari kupitia SMS, hivyo IOM imepata mshirika mkubwa, kampuni ya Digicel ambayo inaweza kutoa habari kwa wakazi wanaokabiliwa na hatari za vimbunga."

IOM inaanzisha pia kipindi cha redio cha kila siku kinachozingatia kuelimisha juu ya hatari za majanga wakati wa msimu wa kimbunga.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud