Ban Ki-moon awaombea heri waliokwama kwenye machimbo nchini Chile
Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amewaombea heri manusuru wanaoendelea kukwama katika machimbo moja ya migodi nchini Chile akisema kuwa anaamini wataopolewa wakiwa bado salama.
Wachimbaji hao wapatao 33, walikwama kwenye mgodi mmoja ulioko Kaskazini mwa Chile wakiwa kwenye harakati za utafutaji madini, lakini baadaye iligundulika kuwa licha ya kukwama kwenye umbali mrefu zaidi,hata hivyo bado walikuwa hai.
Msemaji wa Katibu mkuu huyo Martin Nesirky amekaririwa akisema kuwa
Ban Ki-moon amewataka manusura hao waendelee kujipa matumaini hasa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia na kuwaomba wasife moyo kwani anaamini iko siku watakuja kuondoka kwenye kadhia hiyo.
Vyombo vya habari vinasema kwamba huenda ikachukua muda wa miezi kadhaa hadi kuwafikia mahali walipo manusura hao ambao wamenasa umbali wa mamia ya mita chini ya ardhi, wakati upande mmoja wa machimbo ulipoporomoka na kuwakinga washindwe kutoka tena.