Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito watolewa wa kuhakikisha kuwepo kwa usawa wa kimaendeleo nchini Vietnam

Wito watolewa wa kuhakikisha kuwepo kwa usawa wa kimaendeleo nchini Vietnam

Huko Vietnam ikizidi kupiga hatua za kimaendeleo kukabiliana na umaskini kwa miongo miwili iliyopita kumetolewa wito wa kuwepo kwa juhudi zaidi na kujumuishwa jamii maskini.

Akikamilisha ziara ya siku tisa nchini Vietnam mtaalamu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu na umaskini Magdalena Sepúlveda, amesma kuwa tatizo la umaskini linaweza pia kukabiliwa kutokana na kuwepo kwa haki. Mtaalamu huyo amesema kuwa kila mmoja nchini Vietnam anastahili kupata haki zikiwemo za kichumi, kitamaduni, kijamii na kisiasa akisema kuwa hakuna eneo au makundi ya watu wanaostahili kuachwa nyuma katika maendeleo. Bi Sepulveda alisikitishwa zaidi na hali kubwa ya umaskini miongoni mwa jamii ndogo ambazo zinaishi kwenye maeneo ya mbali vijijini ambazo hukumbwa na matatizo makubwa na kupata huduma muhimu.

Bi Sepúlveda pia ametoa wito wa kuwepo uwazi , uwajibikaji na uwakilishi wa jamii zote katika masuala ya nchi ili kutoa nafasi kwa makundi mengine kueleza matatizo yanayowakabili . Aidha ametaka kutolewa na nafasi kwa kila mmoja kufahamu haki yake na jinsi anavyoweza kupata haki hiyo.