Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaalani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari Indonesia

UNESCO yaalani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari Indonesia

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO amelaani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari mmoja wa Indonesia na ameitaka mamlaka inayohusika kuwaleta katika mkono wa sheria wale wote waliohusika kwenye mauwaji hayo.

Muungano wa vyombo vya habari Kusini mwa Asia SEAPA umesema kuwa mwandishi huyo wa habari alishambuliwa na kuchomwa na vitu vyenye nchi kali na wanajiji hao na baadaye alipoteza maisha akiwa hospitalini kutokana na majeraha makubwa aliyopata.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova pamoja na kuelezea masikitiko yake juu ya kadhia hiyo ameseama kuwa waandishi wa habari ni watu ambao wanapaswa kuhakikishia usalama wao wakati wowote wawapo kazini.