Idara ya UM inawafunza wakufunzi juu ya kupunguza hatari za janga
Warsha ya kutoa mafunzo kwa wakufunzi juu ya namna ya kupunguza hatari za majanga imefunguliwa huko Kenya kwa matumaini kwamba wanaoshiriki watatumia masomo waloyapata kwengineko barani Afrika.
Mkuu wa ofisi ya Afrika ya ISDR Pedro Basabe anasema matokeo ya mafunzo hayo ni kubuni tovuti ya kusambaza habari juu ya kupunguza hatari za majanga kwa jamii na hivyo kuongeza maarifa yao na kuweza kukabiliana vyema zaidi na maanga asili.
Warsha hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwafunza wakufunzi katika kiwango cha viijini, ambao watarudi kuwafunza jamii juu ya jinsi ya kutumia uwezo wao na rasilmali kukabiliana na ajali kabla ya kuwa majanga