Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waitaka Urusi kufanya hima kulinda haki za jamii za kiasili

Umoja wa Mataifa waitaka Urusi kufanya hima kulinda haki za jamii za kiasili

Umoja wa mataifa umeishauri urusi kulinda haki za jamii za kiasili nchini mwake .

Mtaalamu wa masuala yanayohusiana na haki pamoja na uhuru wa watu wa asili katika nyanja za kiuchumi, afya na lugha James Anaya amesema kuwa nyingi ya jamii za kiasili nchini Urusi zinaendelea kukabiliwa na matatizo ya kupata kikamilifu haki zao.

Hata hivyo Anaya ameipongeza Urusi kwa kujitolea kuinua maisha ya jamii hizo hasa kwa kuendeleza utamaduni wao na kujumuisha kwenye utoaji wa maamuzi. Mtaalamu huyo amesema pia kuwa kutekelezwa kwa sheria zilizopo zinazoruhusu jamii hizo kupata haki zao linatajwa kuwa suala linalostahili kutatatuliwa. Anaya anatoa ripoti yake baada ya ziara yake nchini Urusi mwezi oktaba mwaka uliopita ambapo alizitembelea jamii zinazotambuliwa na serikali kama ndogo na za kiasili zilizo na watu wasiozidi 50,000.

Mtaalamu wa masuala yanayohusiana na haki pamoja na uhuru wa watu wa asili katika nyanja za kiuchhumi, afya na lugha James Anaya amesema kuwa nyingi ya jamii za kiasili nchini urusi zinaendelea kukabiliwa na matatizo wa kupata kikamilifu haki zao.