UNAMID inapeleka ujumbe kuchunguza mapigano ya kikabila Darfur

UNAMID inapeleka ujumbe kuchunguza mapigano ya kikabila Darfur

Mpango wa kulinda amani Darfur wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID unatuma ujumbe katika vijiji kadhaa nje ya mji wa Kass kusini mwa Darfur kufuatia kuzuka kwa mapigano ya kikabila.

UNAMID inasema watu 25 wamearifiwa kuuawa katika machafuko hayo yaliyoanza Jumatatu wiki hii kati ya makundi ya kikabila ya Rizeigat na Misseriya.

Mpango huo wa UNAMID pia umeripoti kwamba makundi ya misaada yameruhusiwa kuingia kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma kwenye jimbo la Darfur. Makundi hayo yalizuiliwa na serikali ya Sudan kuingia Kalma kutokana na sababu za kiusalama.