Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Agosti 19 ni siku ya kimataifa ya wahisani

Agosti 19 ni siku ya kimataifa ya wahisani

Agosti 19 ni siku ya kimataifa ya wahisani ambayo ni maalumu kwa ajili ya waliopoteza maisha yao kwakitoa huduma ya kuwasaidia wengine.

Siku hii ambayo itaambatana na hafla mbalimbali duniani pia inaadhimishwa kutoa msisitzo wa mahitaji ya kibinadamu na changamoto zilizopo duniani kote kama vile vitisho dhidi ya wafanyakazi wa misaada katika maeneo ya vita, changamoto za kuwafikishia msaada wanaouhitaji na ugumu wa kutekeleza masuala ya misaada kutokana na sababu mbalimbali.

Sababu hizo ni pamoja na ongezeko la bei ya chakula, msukosuko wa soko la dunia, upungufu wa maji na mabadiliko ya hali ya hewa. Kuna malengo matatu katika kuadhimisha siku hiyo mwaka huu.

Malengo hayo ni kutanabaisha mahitaji ya msaada wa kibinadamu duniani, kulezea kwa lugha nyepesi kuhusu kazi za uhisani ni nini na kuwakumbuka waliopeteza maisha yao wakihudumia wengine.