Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kifungo cha afisa wa Khmer Rouge kiongezwe:waendesha mashitaka

Kifungo cha afisa wa Khmer Rouge kiongezwe:waendesha mashitaka

Waendesha mashitaka kwenye mahakama ya uhalifu ya Cambodia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya wametangaza kwamba watawasilisha ombi la kuongezwa kifungo jela cha mkuu wa zamani wa magereza wa Khmer Rouge.

Kaing Guek Eav maarufu kama duch alikutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miaka 30 tarehe 26 Julai mwaka huu kwa uhalifu alioutekeleza alipokuwa mkuu wa gereza S-21, na majaji wakaamua kwamba Guek Eav atatumikia kifungo cha miaka 19 baada ya kupunguza miaka ambayo tayari alikuwa kizuizini. Waendesha mashitaka hao wamesema wana mpango wa kukata rifaa ya hukumu yake kwa misingi kwamba huku hiyo imeshindwa kuwiana na uhalifu uliotekelezwa na afisa huyo wa zamani wa Khmer Rouge.

Kwa mtazamo wao Duch anatakiwa kuhukumiwa tofauti kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuwafanya watu watumwa, kuwafunga, kuwatesa, ubakaji,kuwauwa na makosa mengine ya kikatili.

Manasema makosa hayo yasingejumuishwa na pili kipengele cha uhalifu wa kuwafanya watu watumwa hakifafanuliwa vizuri kwenye hukumu ya awali na hivyo kushindwa kumtia hatiani Duch kwa kuwafanya watumwa asilimia kubwa ya wafungwa kwenye gereza hilo la S-21.