Skip to main content

Baada ya kuzuru Pakistan Ban atoa ahadi ya msaada zaidi huku WHO ikionya juu ya magonjwa ya mlipuko

Baada ya kuzuru Pakistan Ban atoa ahadi ya msaada zaidi huku WHO ikionya juu ya magonjwa ya mlipuko

Shirika la afya duniani WHO linasema wakati mamilioni ya waathirika mwa mafuriko nchini Pakistan wakiendelea kusubiri msaada wa dharura sasa maradhi ya mlipuko kama kuhara yanatishia usalama wa watu hao.

Shirika hilo linasema katika jimbo la Khber Pakhtunkhwa watu 3807 wamewsili katika kituo cha afya wakisumbuliwa na maradhi ya kuhara kutokana na kutopata maji safi na salama ya kunywa, hiyo ikiwa ni asilimia 17 ya wagonjwa wote, huku wengizi 3255 sawa na asilimia 15 wanasumbuliwa na magonjwa ya mfumo wa hewa.

Magonjwa ya ngozi pia yamearifiwa kusambaa kwa asilimia 19, ambapo watu 4222 wanatibiwa hivi sasa. Majimbo mengine yaliyoathirika na maradhi hayo kwa mujibu wa WHO ni Punjab, Balouchstan, na Sind na hivi sasa kuna uvumi wa kuzuka kipindupindu katika eneo la Mingora kwenye wilaya ya Swat. Akizuru Pakistan jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaahidi watu wan chi hiyo kuwa Umoja wa Mataifa uko pamoja nao.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Mbali ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali, mashirika mengine ya kimataifa na serikali wanafanya kila liwezekanalo ili kuwasaidia mamilioni ya waathirika wa mafuriko hayo.