Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaendesha zoezi la kukabiliana na maradhi Asia

UM unaendesha zoezi la kukabiliana na maradhi Asia

Umoja wa Mataifa leo umeanza siku nne za zoezi la maandalizi ya kukabiliana na mlipuko wa maradhi Kusini Mashariki mwa Asia, kwa lengo la kuongeza uwezo wa kanda hiyo kudhibiti hali itakapojitokeza.

Waandaaji wa zoezi hilo linalofanyika mjini Phinom penh Cambodia wanasema ni mara ya kwanza mataifa mbalimbali yanaungana pamoja katika juhudi za kukabiliana na mlipuko wa maradhi kwenye sekta mbalimbali kwenye kanda hiyo.  Kwa mujibu wa Nhim Vanda afisa wa udhibiti wa majanga katika serikali ya Cambodia anasema zoezi hilo litatoa fursa kwa sekta mbalimbali kujiandaa kwa dharura katika ukanda mzima.

Katika zoezi hilo watajifunza kuhusu mlipuko wa maradhi na athario zaake katika huduma muhimu mfano nishati, usafiri na huduma ya afya. Na itazilenga nchi zote tano za Kusini Mashariki mwa Asia. Nchi za Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos, Malaysia, Myanmar, Ufilipino, Singapore, Thailand na Vietnam wanashiriki zoezi hilo , ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu.