Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii za watu wa asili zinastihili haki sawa na jamii yeyote ile duniani: UM

Jamii za watu wa asili zinastihili haki sawa na jamii yeyote ile duniani: UM

Wiki hii Umoja wa Mataifa na nchi mbali mbali duniani wameungana kuadhimisha siku ya kimataifia ya watu wa asili, na UM umehimiza kwamba nchi zote duniani lazima ziheshimu na kutekeleza haki za msingi za watu wa asili.

Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii, Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amesema watu wengi na jamii nyingi za watu wa asili bado wanadhulumiwa, haki zao za binadamu zinakiukwa, kwingineko hawashirikishi katika ngazi za maamuzi na ndio wanaokabiliwa na matatizo mengi ya kiafya. Hivyo amezitolea wito nchi zote kuhakikisha kwamba zinatumia sera zake kuzihushisha jamii za watu wa asili katika masuala mbalimbali.

Kwa upande wa Afrika kuna jamii nyingi za watu wa asili na miongoni mwao ni jamii ya waturkana kutoka kaskazini mwa Kenya ambao mwandishi wetu Jason nyakundi amezungumza na baadhi yao katika taarifa hii maalumu.