Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa UNESCO ameelezea hofu yake juu ya kifo cha mwandishi habari wa India

Mkurugenzi wa UNESCO ameelezea hofu yake juu ya kifo cha mwandishi habari wa India

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kutetea uhuru wa vyombo vya habari leo ameelezea hofu yake juu ya kifo cha mwandishi wa habari wa India Hem Chandra Pandey.

Mwandishi huyo pamoja na kiongozi wa Kimao waliuawa mapema mwezi huu katika Purukushani na polisi kwenye jimbo la Andthra Pradesh.

Mkuu huyo wa UNESCO Irina Bokova amesema nina wasiwasi na mazingira yaliyosababisha kuuawa kwa Pandey na ninaitaka serikali kuchukuza mazingira ya kifo hicho .

Bwana Pandey mwenye umri wa miaka 30 alikuwa mwandishi wa kujitegemea aliyefanya kazi na magazeti mengi ya kila siku ya Kihindi. Yeye na kiongozi wa Kimao Cherukuri Rajkumar waliuawa tarehe pili ya mwezi huu.