Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la UM limealaani kuzamishwa kwa meli ya Jamhuri ya Korea hivi karibuni

Baraza la usalama la UM limealaani kuzamishwa kwa meli ya Jamhuri ya Korea hivi karibuni

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limealaani kuzamishwa kwa meli ya Jamhuri ya Korea hivi karibuni huku likisisitiza haja ya kuzuia mashambulio zaidi dhidi ya taifa hilo la Asia mashariki na ukanda mzima.

Watu 46 waliokuwa ndani ya meli ya Cheonan walikufa baada ya meli hiyo kuzama mwishoni mwa mwezi Machi. Uongozi mjini Seoul ulitoa ripoti ya uchunguzi wa kimataifa mwezi Mai iliyohitimisha kwamba meli hiyo ilizamishwa na kombora la topido lililovurumishwa na jirani zao wa Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea,au Korea Kaskazini (DPRK).

Taarifa ya Rais wa baraza hilo imepitishwa na wajumbe wote 15 wa baraza na kusema mashambulio kama hayo yanahatarisha amani na usalama kwenye ukanda mzima na nje.

Rais wa baraza kwa mwezi huu ni balozi wa Nigeria U Joy Ogwu

(SAUTI YA BALOZI U. JOY)

Baraza limetoa wito wa kuchukuliwa hatua muafaka na za amani dhidi ya waliohusika na tukio hilo, kwa lengo la kumaliza mvutanno huo kwa njia ya amani. Na pia limeelezea hofu yake juu ya mtazamo wa matokeo ya uchunguzi wa kundi la kiraia na kijeshi ambao umehitimisha kwamba DPRK walihusika kuzamisha meli ya Cheonan.