Skip to main content

Afghanistan yakabiliwa na tatizo kubwa la matumizi ya dawa za kulevya

Afghanistan yakabiliwa na tatizo kubwa la matumizi ya dawa za kulevya

Ripoti ya utafiti wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na dawa na uhalifu UNIDOC kinasema Afghanistan inakabiliwa na tatizo kubwa la matumizi ya dawa za kulevya.

Utafiti huo ulioishirikisha serikali ya Afghanistan umebaini kuwa nchini humo watu wapatao milioni moja wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 64 wanasumbuliwa na maradhi ya utumiaji dawa za kulevya kupita kiasi. Hii ni asilimia nane ya watu wote na ni mara mbili ya kiwango cha chini cha kimataifa cha matumizi ya dawa hizo.

Mkurugenzi wa UNIDOC Antonio Maria Costa amesema baada ya miongo mitatu ya athari za vita, kupatikana kwa bei chee kwa dawa za kulevya na ukosefu wa matibabu, kumesababisha tatizo kubwa la wagonjwa wa kutumia dawa hizo nchini Afghanistan.