Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Korea zote zimewasilisha hoja zao kwenye baraza la usalama kuhusu sakata ya meli

Korea zote zimewasilisha hoja zao kwenye baraza la usalama kuhusu sakata ya meli

Seoul imeutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ikiilaumu Pyongyang kuhusika na kuzamisha meli ya Cheonan ya Korea Kusini mwezi Machi na kuua mabaharia 46.

Lakini Korea Kaskazini imekanusha kuhusika na sakata hiyo na kusema wao ni waathirika tuu. Baada ya kusikiliza pande zote ,maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema wanahofia kuhusu suala hilo na wanahitaji kulijadili zaidi. Katika taarifa yake Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka pande zote kutichukua hatua zozote zitakazoleta mvutano katika eneo hilo.

Korea ya Kusini imewasilisha ushahidi kwa kutumia power point wanaosema unaonyesha meli yao ilizamishwa na torpedo ya Korea Kaskazini.Mwakilishi wa Korea Kusini Yoon Duk-yong ameliambia baraza la usalama wanamatumaini kwamba baraza hilo litachukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini. Nayo Korea ya Kaskazini imedai kutaka kuzuru eneo la tukio la kuzama kwa meli hiyo na kwa mara nyingine imeendelea kukanusha madai ya Korea Kusini na kuyaita ni ya kughushi.