Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa siasa wa UM amekwenda Sri Lanka kwa mazungumzo ya haki na maridhiano

Mkuu wa siasa wa UM amekwenda Sri Lanka kwa mazungumzo ya haki na maridhiano

Afisa wa juu wa masuala ya siasa katika Umoja wa Mataifa leo anawasili Sri Lanka kaama sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kulisaidia taifa hilo la Asia kukabiliana na athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka jana.

Bwana B.Lynn Pascoe mwakilishi wa masuala ya siasa atakuwa na mazungumzo na Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaska, maafisa wengine wa serikali, wapinzani na wawakilishi wa vyama vichache, viongozi wa Tamil, wawakilishi wa vyombo vya habari na jumuiya za kijamii. Pia bwana Pascoe anatarajiwa kukutana na mratibu wa masuala ya Umoja wa Mataifa nchini humo Neil Buhne, wafanyakazi wa UM na msemaji wa Umoja wa Mataifa nchini humo Farhan Hag.

Ziara yake italenga maridhiano ya kisiasa, haki za binadamu na makazi ya kudumu kwa wakimbizi wa ndani. Umoja wa Mataifa pia unaunda jopo la wataalamu kama sehemu ya kufuatilia ukiukaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu kufuatia kumalizika mwaka jana kwa vita vya wenywe kwa wenyewe.