Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya UM ya haki za binadamu imesaini tena makubaliano na Nepal

Ofisi ya UM ya haki za binadamu imesaini tena makubaliano na Nepal

Ofisi za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zimekubali ombi la serikali ya Nepal la kupunguza uwepo wake nchini humo kwa kufunga baadhi ya ofisi zake nje ya Kathmandu katika miezi ijayo.

Chini ya makubaliano hayo ofisi za haki za binadamu zitaendelea kuwa na uhuru wa kutembea na kuendelea kutekeleza wajibu wake katika nchi nzima. Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amekaribisha hitimisho la makubaliano hayo na serikali ya Nepal kwa kuongeza miezi mingine 12 na jukumu la ofisi zao.

Ofisi za haki za binadamu nchini humo zimekuwa zikifuatilia na kuripoti masuala ya haki za binadamu na kutoa mafunzo na msaada wa kiufundi kwa taasisi za serikali na jumuiya za kijamii tangu zilipoanzishwa nchini Nepal mwaka 2005.