Skip to main content

ILO imetoa ripoti ya hali ya wafanyakazi eneo la Wapalestina linalokaliwa

ILO imetoa ripoti ya hali ya wafanyakazi eneo la Wapalestina linalokaliwa

Shirika la kazi duniani ILO linasema hali ya wafanyakazi katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa imeimarika kiuchumi.

Hayo yamo katika ripioti ya mwaka huu ya shirika hilo ambayo inasema licha ya hatua ilityopigwa bado hali ni tete hususan Gaza. Ripoti hiyo imezingatia sana kukua japo kiasi kwa uchumi na ongezeko la ajira ambalo kwa viwango vya kimataifa bado ni dogo. Athari za Israel kulifunga kabisa eneo la Ukanda wa Gaza ni kwamba uchumi umedumaa na mgawanyiko wa rasilimali baina ya gaza na ukingo wa Magharibi unatofautiana.

Hali ya uchumi, kijamii na maisha ya watu katika eneo la Wapalestina linalokaliwa vinafanya kuwe na mazingira mabaya na haki za wafanyakazi kuendelea kukiukwa kila siku, amesema mkurugenzi wa ILO Juan Somavia akiongeza kuwa kukosekana kwa fursa nyingine kumelazimisha Wapalestina wengi kutafuta ajira katika uchumi usio rasmi ambako malipo ni madogo na haki zao hazilindwi.