Wataalamu wa UM wataka DRC kuhushisha wachunguzi huru katika mauaji ya Chebeya

Wataalamu wa UM wataka DRC kuhushisha wachunguzi huru katika mauaji ya Chebeya

Serikali ya Congo pia imewatia mbaroni watu kadhaa baada ya Floribert Chebeya Bahizire kuuawa na maiti kukutwa ndani ya gari lake, na kutoweka hadi sasa kwa derebva wake Fidele Bazana Edadi.

Wataalamu hao ambao wanataka pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwahusisha wachunguzi binafsi wa kimataifa katika uchunguzi wa mauaji hayo, wamesema kushindwa kuwakamata na kuwachukulia hatua waliohusika itakuwa ni pengo kubwa na kurudisha nyuma juhudi kubwa zilizopigwa na serikali. Wametaka pia wachunguzi hao binafsi kushiriki katika kumsaka dereva Edadi ambaye hadi sasa hajulikani alipo.