Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM kuongeza muda wa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini.

Baraza la Usalama la UM kuongeza muda wa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi leo kwa pamoja limeafikiana kuongeza muda wa wataalamu wanaoshughulika na vikawazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya serikali ya Korea Kaskazini kwa mwaka moja.

Baraza hilo pia limehimiza mataifa, mashirika wahusika wa Umoja wa Mataifa na wahusika wengine wote kuipa kamati hiyo ya wataalamu taarifa zozote walizonazo kuhusiana na utekelezaji wa hatua zilizopipitishwa na azimio la Umoja wa Mataifa nambari 1718 la mwaka mwaka wa 2006 na azimio nambari 1874 la mwaka jana.

Azimio nambari 1718, liliidhinishwa na baraza hilo baada ya serikali ya Korea Kaskazini kudaiwa kufanya majaribio ya nyuklia Oktoba 2006 na hivyo kupelekea baraza la usalama kuiwekea vikwazo nchi hiyo pamoja na baadhi ya watu wanaounga mkono programu ya kijeshi.