Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon ataka itikadi kali zikomeshwe kote duniani

Ban Ki-moon ataka itikadi kali zikomeshwe kote duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito kwa watu kukataa itikadi kali. Na amesema nchi zaidi ya 100 wanachama wa kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) zinajukumu kubwa katika kuchagiza maelewano katika jamii.

Amesema tunahitaji kuwawajibisha ambao wanachochea hisia kali na kupotosha, au watu wanaowadhalilisha na kuwashawishi wengine kwa misingi ya kushinda uchaguzi.

Bwana Ban ametoa ujumbe huo kwa njia ya video kwa wanachama wa NAM wanaokutana mjini Manila Philipines kwa ajili ya mazungumzo ya muingiliano wa kidini kwa ajili ya amani na maendeleo.

Pia ameomba msaada kutoka Nam kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuondoa mtafaruku baina ya mataifa, tamaduni na dini.

Ban amesema amani, maendeleo na haki za binadamu vyote vinategemea kuwepo maelewano na kuheshimiana katika jamii.