Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kutafuta mbunu kukomesha usajili wa watoto vitani

UNICEF kutafuta mbunu kukomesha usajili wa watoto vitani

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto, UNICEF linatafuta mbinu za kuwasaidia watoto wasisajiliwe katika vita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Warsha ambayo imeandaliwa na serikali ya Chad kwa kusaidiwa na UNICEF umefunguliwa katika mji mkuu wa N'Djamena hii leo ili kumaliza usajilishaji kwa watoto unaofanywa na serikali na makundi yenye silaha.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Chad, Marzio Babile amesema maelfu ya watoto wanashiriki mapigano yanayoathiri nchi ya Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan na kuongeza kuwa watoto hawana nafasi katika mapigano na kusajiliwa kwao ni tatizo ambalo linahitaji kukomeshwa mara moja.