Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna msichana anayestahili kunyimwa haki ya elimu:Naibu mkuu wa haki

Hakuna msichana anayestahili kunyimwa haki ya elimu:Naibu mkuu wa haki

Naibu mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kyung-Wha Kang amesema kutambua haki ya elimu ni muhimu kwa wanawake kuweza kufurahia haki za binadamu.

Hayo ameyasema leo kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva ambao unajadili haki za wanawake, na amesisitiza kwamba asiwepo hata msichana mmoja atakayeendelea kunyimwa haki yake ya elimu.

Amesema wanawake kutojumuishwa katika elimu ni kuwatenga na kuwabagua na ni jambo ambalo halikubaliki.

(SAUTI YA  KYUNG GENEVA)