UM umebaini hali mbaya iliyoko kwenye mahabusu nchini Papua New Guinea

UM umebaini hali mbaya iliyoko kwenye mahabusu nchini Papua New Guinea

Mahabusu nchini Papua New Guinea wanashikiliwa kwa muda mrefu na katika mazingira mabaya yasiyokubakila kwa binadamu yanayojumuisha unyama, udhalilishwaji na adhabu kali.

Tathimini hiyo imetolewa na mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya utesaji Manfred Nowak ambaye amefanya ziara Papua New Guinea kuanzia tarehe 14 hadi 25 ya mwezi huu wa Mai kwa mwaliko rasmi wa serikali.

Bwana Nowak ameelezea hofu yake kuhusu kupigwa kwa mahabusu wanapokamatwa na polisi, saa za mwanzo wanaposhikiliwa na wakati wanapohojiwa. Amesema hii ni hali ya kila wakati inayofanywa na polisi na kuna ushahidi wa madaktari. Pia amebaini kwamba katika vituo vingo vya polisi kikiwepo cha Highlands mahabusu wanalazimishwa kulala sakafuni bila hata blanketi za kujifunika na hali ya usafi ni mbaya mno.

Ameshuhudia mahabusu walilazimishwa kukojoa kwenye chupa na kujisaidia haja kubwa kwenye mifuko ya plastiki ambayo inakusanywa mahali pamoja na mahabusu wa kike. Ameishukuru serikali kwa ushirikiano alioupata kwa kamishina wa polisi uliomuwezesha kuzuru mahabusu hizo bila taarifa na kuzungumza na mahabusu.