Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM imeweka vituo kuwasaidia waliokwama Niger wakitaka kwenda Ulaya

IOM imeweka vituo kuwasaidia waliokwama Niger wakitaka kwenda Ulaya

Vituo viwili katika eneo la Kaskazini mwa Niger la Agadez vinazidi kuwapa usaidizi ya kibinadamu kwa wahamiaji wanaojaribu kwenda Ulaya na wale waliopotea njia wakijaribu kurudi nyumbani kutoka Ulaya, na waliorudishwa kwa nguvu kutoka mataifa ya jirani ya Algeria na Libya.

Vituo hivyo vinavyofadhiliwa na serikali ya Italy inawapa watu hao mahala pa kulala ya muda, chakula, nguo na vifaa vya usafi na huduma ya afya sawa na kuwanoya hatari ya uhamiaji haramu.

IOM, imekuwa  ikishirikiana na wadau wengine kama shirika la msalaba mwekundu nchini Niger, utawala wa kitaifa na wa mashinani katika wilaya ya Dirkou na Arlit na wawakilishi wa shirika la ushirikiano wa Italia nchini Chad.