Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi wa UM umebaini serikali ya Pakistan ilishindwa kumlinda Benazir Bhutto

Uchunguzi wa UM umebaini serikali ya Pakistan ilishindwa kumlinda Benazir Bhutto

Ripoti ya tume binafsi ya uchunguzi wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto imehitimisha kwamba serikali ya Pakistan ilishindwa kumlinda Bi Bhutto licha ya vitisho dhidi ya maisha yake.

Benazir Bhutto ambaye alirejea Pakistan Oktoba 2007 aliuawa tarehe 27 desemba mwaka huohuo katika shambulio la mtu wa kujitoa muhanga wakati akitoka kwenye kampeni mjini Rawalipindi, watu wengine 24 waliuawa na wengine 91 kujeruhiwa.

Balozi Heraldo Munoz wa Chile aliyeongoza uchunguzi huo amesema uchunguzi wao umekabiliwa na vikwazo hasa vya kuwatambua na kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria, lakini serikali ya Pakistan inapaswa kulaumiwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameikaribisha ripoti hiyo na kusema itachangia kumaliza makosa ya kisiasa kama hayo na kuupa nguvu utawala wa sheria wa Pakistan.