Skip to main content

Idadi ya waliokufa katika tetemeko China ikiongezeka madawa na mahema vimekuwa hadimu

Idadi ya waliokufa katika tetemeko China ikiongezeka madawa na mahema vimekuwa hadimu

Shirika la afya duniani WHO linasema idadi ya waliokufa imefikia 617 na wengine zaidi ya elfu tisa wamejuruhiwa kwenye tetemeko la ardhi katika mji wa Yushu jimbo la Qinghai Uchina.

Watu wengine wapatao laki moja wanahitaji kuhamishiwa katika maeneo salama. Hata hivyo kumekuwa na hofu juu ya ukosefu wa mahema, vifaa vya matibabu, madawa na madaktari.

Hivi sasa serikali ya Uchina inapeleka jopo la wahudumu wa afya na tani sita za madawa na vifaa vya matibabu.

WHO imesema iko tayari kusaidia kama serikali ya Uchina itahitaji msaada. UNICEF kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa inajiandaa kupeleka msaada kwa watoto walioathirika na tetemeko hilo