Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO inasema volcano iliyoanza kuripuka Jumatano Iceland itaendelea

WMO inasema volcano iliyoanza kuripuka Jumatano Iceland itaendelea

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limesema mlipuko wa volikano ulioanza siku ya Jumatano nchini Iceland utaendelea ingawa kiwango cha jivu kimepungua.

Limesema hata hivyo mlipuko huo bado unachukuliwa kwa uzito mkubwa na athari zake hususani vumbi la jivu zitaendelea kwa muda. WMO imesema ni vigumu kutabiri lini ndege zitaanza safari lakini kama mlipuko huo utaendelea basi ndege haziwezi kusafiri.

Nalo shirika la afya duniani WHO limesema bado halijafahamu athari za kiafya zitakazosababishwa na volcano hiyo, japo limesema kama jivu litazidi basi linaweza kuwa na athari kubwa hasa kwa wagonjwa wa athma na wenye matatizo ya kupumua.