Skip to main content

Ban Ki-moon ameshtushwa na kifo cha Rais wa Poland na maafisa wengine

Ban Ki-moon ameshtushwa na kifo cha Rais wa Poland na maafisa wengine

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ameelezea kushtushwa kwake na ajali ya ndege iliyotokea Smolensk na kumuuwa rais wa Poland, mkewe na maafisa wengine wa serikli.

Ban amesema ni masikitiko na huzuni kwa watu wa Poland.Umoja wa Mataifa uko pamoja nao na serikali ya Poland katika wakati huu mgumu wa majonzi. Ameongeza kuwa amefanya kazi kwa karibu na marehemu Rais Lech Kaczynski ambaye alihudumia watu na taiafa lake kwa moyo wote na juhudi na aliheshimika kote duniani.

Ban amesema kifo chake kina uzito mkubwa hasa kwa wakati kilipotokea akielekea kwenye tukio linalofungua ukurasa mpya wa maridhiano baina ya Poland na Urusi.