Ban Ki-moon ataka utulivu urejee baada ya waandamanaji kuteka jengo la serikali

6 Aprili 2010

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea hofu yake juu ya taarifa kwamba waandamanaji nchini Kyrgyzstan wameteka jengo la serikali.

Ban amewaomba wawe watulivu na kuheshimu utawala wa sheria. Mamia ya watu walioandamana kupinga ongezeko la gharama za gesi na umeme leo wameteka jengo la serikali kwenye mji wa Talas magharibi mwa mji mkuu Bishkek.

Ban amewataka wafanmye mazungumzo kumaliza tafrani hiyo na amesisitiza kuwa wakati uhuru wa kukusanyika ni kitu muhimu katika jamii inayozingatia demokrasia lakini pia utawala wa sheria lazima uheshimiwe.

Bwana Ban alizuru Kyrgyzstan siku ya Jumamosi na kwasisitiza kulinda haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kuongea na kujieleza katika nchi hiyo ya Asia ya Kati.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter