Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yameleta athari kubwa nchini Kenya kwa watu na mali zao.

Mafuriko yameleta athari kubwa nchini Kenya kwa watu na mali zao.

Mafuriko makubwa yameikumba nchi ya Kenya hivi karibuni na kusababisha athari kubwa kwa watu na mali zao katika sehemu mbalimbali.

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni ya Mashariki, Kaskazini mashariki na magharibi mwa nchi hiyo . Zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha, maelfu wameachwa bila makazi na maelfu ya mifugo yameangamia. Mashirikika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yamekuwa msitari wa mbele kutoa msaada wa dharura ikiwemo OCHA, UNICEF na chama cha msalaba mwekundu.

Katika makala yetu ya wiki leo inaangazia mafuriko hayo na athari zake. Mwandishi wetu mjini Nairobi Jason Nyakundi alifunga safari hadi maeneo yaliyoathirika na kutukusanyia aliyoshuhudia ungana naye katika makala hii inayosikika pia kwenye tovuti.