Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la kigaidi lauwa zaidi ya watu 30 mjini Moscow Urusi

Shambulio la kigaidi lauwa zaidi ya watu 30 mjini Moscow Urusi

Mashambulio mawili ya mabomu leo yameukumba mfumo wa usafiri wa treni za chini ya ardhi mjini Moscow Urusi na kukatili maisha ya watu zaidi ya 30 na wengine wengi kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya majanga na dharura Veronika Smolskaya moja ya shambulio hilo linadaiwa kufanywa na mshambuliaji wa kujitoa muhanga. Watu 22 waliuawa kwenye mripuko wa kwanza kwenye stesheni ya Lubyanka katikati ya mji wa Moscow.

Shambulio la pili lilitokea dakika 45 baadaye kwenye stesheni ya Park Kultury ambako watu 12 waliuawa. Idara ya upelelezi ya Urusi imesema wanashuku matukio hayo ni vitendo vya kigaidi.