Skip to main content

Vikwazo dhidi ya Iran itakuwa ajenda kuu kwenye mkutano wa G-8 leo

Vikwazo dhidi ya Iran itakuwa ajenda kuu kwenye mkutano wa G-8 leo

Waziri wa mambo ya nje wa Canada amesema mipango ya nyuklia ya Iran inatia mashaka na ndio itakuwa ajenda kuu kwenye kikao cha mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi nane tajiri duniani G-8.

Bwana Lawrence Cannon amesema atashinikiza kuwekwa kwa vikwazo vigumu zaidi, mawaziri hao wa G-8 watakapokutana jioni ya leo kuanza mkutano wao utakaoendelea hadi kesho Jumanne huko Gatineau Quebec.

Marekani na washirika wake wamekuwa wakiusukuma Umoja wa Mataifa kupitisha duru ya nne ya vikwazo dhidi ya mipango ya nyuklia ya Iran. Iran inaendelea kusisitiza kuwa mipango yake ya nyuklia ni ya amani, lakini serikali za magharibi zinaamini Iran inajiandaa kuunda silaha za atomic.