Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imerejea saada Yemen baada ya miezi minane

UNHCR imerejea saada Yemen baada ya miezi minane

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepata fursa kuingia kwenye jimbo la Saada Yemen kwa mara ya kwanza tangu kuzuka machafuko mwezi Agust mwaka jana.

Mkataba wa amani uliosainiwa Februari 11 mwaka huu baiana ya serikali na waasi unaonekana kutekelezwa. Mji wa Saada unarejea katika hali ya kawaida ingawa kurudi mjini humo kwa idadi kubwa ya watu kunahitaji utulivu, usalama na misaada.

Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ya Yemen wamekutana na viongozi wa jimbo la Saada kujadili mahitaji ya watu jimboni hapo.

Zaidi ya wakimbizi wa ndani laki mbili na nusu wameorodheshwa hadi sasa lakini kutokana na kupanua wigo serikali ya Yemen inaamini kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inafikia laki tatu unusu.