Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inakabiliwa na upungufu wa fedha za kuisaidia Somalia

WHO inakabiliwa na upungufu wa fedha za kuisaidia Somalia

Shirika la afya duniani WHO linakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha katika mradi wake wa dharura wa kuisaidia Somalia.

Hadi sasa asilimia nane tuu ya dola milioni 46 ya fedha za msaada inazohitaji ndio zilizopatikana na zimetolewa na mfuko wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa.

WHO inasema iko katika hali mbaya na inafikiria kupunguza shughuli zake katika baadhi ya maeneo nchini humo, lakini inahofia athari zitakazojitokeza kutokana na kufanya hivyo hasa katika upande wa afya, Paul Garwood ni afisa wa WHO