Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti inakabiliwa na matatizo makubwa ya mazingira

Haiti inakabiliwa na matatizo makubwa ya mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la linalohusika na mazingira UNEP limesema Haiti inakabiliwa na changamoto kubwa za mazingira baada ya tetemeko la ardhi la Januari 12.

Kabla ya tetemeko Haiti ilikuwa ni nchi yenye matatizo ya mmomonyoko wa udongo katika eneo la Carebian, sasa hali hii imekuwa mbaya zaidi baada ya tetemeko. Miongoni mwa changamoto zinazoikumba nchi hiyo hivi sasa ni jinsi ya kutupa kifusi, mabaki ya vifaa vya matibabu na kurejesha katika hali ya kawaida mfumo wa usafi ambao uliharibika kabisa.

Wakati zaidi ya watu milioni moja wameondoka mji mkuu Port-au-Prince na kwenda vijijini hofu ni juu ya rasilimali zilizoko vijijini huko ambazo hazitoshelezi wimbi hilo la watu