Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ongezeko la wanawake kumiliki ardhi ni muhimu sana:FAO

Ongezeko la wanawake kumiliki ardhi ni muhimu sana:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema ongezeko la wanawake katika umilikaji ardhi ni muhimu sana hasa katika mapambano dhidi ya umasikini na njaa.

Limesema hata hivyo usawa wa kijinsia katika umilikaji ardhi bado ni tatizo kubwa katika nchi nyingi licha ya kiwango cha maendeleo walichonacho.

Kwa mujibu wa takwimu za FAO, sera hii inajadili sababu zinazowazuia wanawake kuweza kumiliki ardhi. Pia inaainisha mapendekezo kadhaa ambayo yatasaidia kuwa na sera nzuri ambazo zitaliangalia suala hili na kulipatia ufumbuzi.